-Je una msongo wa mawazo ambao
unashindwa kuuepuka? Katika hali ya kawaida ukiushika kwa kuubana mkono wako
kwa sekunde kadhaa na kuuachilia, utagundua ni jinsi gani kuubana mkono wako
kunavyochosha.
Kushikilia kitu unatumia nguvu
nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni
misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika maisha na mengineyo.
Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi
kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo.
‘’Kwanini tusitue mzigo huu wa
msongo wa mawazo?’’
Kuna sababu nyingi za mtu
kutoepukana na msongo wa mawazo, zikiwemo za kihisia (challenging emotions) na
mazingira yanayomzunguka (watu, mali nk).
Mfano; -Unaweza kuogopa kuvunja
uhusiano wenu wa kimapenzi na mwenza wako kwasababu unaogopa kuwa mpweke utakapokuacha.
--Unaweza kuogopa kuacha au
kufukuzwa kazi kwasababu una wasiwasi wa kukosa kazi mahali pengine hapo
baadae au kupata matatizo ya kifedha.
-Swala la msingi hapa ni kujua namna
ya kumudu hisia (emotional intelligence) na mawazo yako katika hali ngumu
uliyonayo. Huwezi pata jawabu sahihi la matatizo yako mpaka uache kufikiria sana
kwanini au imekuaje umepata matatizo yanakusibu na uhamishe mawazo yako katika
kutafuta ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. Ninachosisitiza hapa, tumia muda na
nguvu nyingi kufikiria suluhu au ufumbuzi wa matatizo yako kuliko matatizo
uliyonayo.
Utakapohamisha mawazo yako kwenye
kupata ufumbuzi, ni rahisi kufunguka kihisia na kiakili na kupata afadhali katika
kupunguza msongo wa mawazo.
-Katika mifano ya matatizo niliyotoa hapo awali
ukiwemo wa kuogopa kuachwa na mpenzi wako utaweza kutatua na kupunguza msongo wa mawazo kwa kusema,..’’Naondoa wasiwasi
wangu wa kuwa mpweke kwa sasa.’’ Neno KWA SASA husaidia kupunguza msongo wa
mawazo kwa wakati huo kwa kukukumbusha kuwa mambo yote hubadilika. Hali ya
ukame ya sasa haimanishi itadumu mpaka masika.
Kubadilika ni swala la kibinadamu,
mtu huweza kubadilika kila mara kulingana na msukumo wa ndani yake (hisia na
akili zake) au shinikizo la kimazingira ya
nayomzunguka. Kwa kawaida mtu mwenye
kushikilia sana matatizo yake sana kiakili hufanya mambo kuwa magumu zaidi
kuliko yule aliyeamua kutua mzigo wa msongo wa mawazo.
0 comments:
Post a Comment