Monday, June 17, 2013

Ukweli kuhusu Mr Nice Kufukuzwa Grandpa Record huu Hapa

Baada ya story nyingi kutapakaa, kupitia mitandao mbali mbali hasa ya nchini Kenya, kuwa msanii Mr Nice ametemwa na record iliyokuwa ikimsimamia kazi zake (Grandpa Recods) iliyoko jijini Nairobi kwa kisa cha yeye kupenda pombe, wanawake na kupigana hovyo, kitu kinachopelekea kuchafua picha ya kampuni hiyolakini pia kusahau majukumu yake anayotakiwa kuyakamilisha kama msanii . 255 imeongea na CEO wa Grandpa "Refigah" amethibitisha kuachana na Mr Nice lakini amekanusha sababu zilizotajwa za yeye kuachana na Mr Nice

kuna sababu ndio zilizopelekea kuachana na Mr Nice, la msingi ni msanii hawezi kuwa na management mbili, hawezi kusign contract mbili bila kusema kuhusu contract hiyo nyingine, alikuwa na contract na Sallam pamoja na Lmar na iko active, so sisi kama company tumeamua hapna, tumesitisha kisheria.

kuhusu kusema kuwa wameachana na Mr Nice kwasababu ya ulevi ugomvi na wanawake, amesema kuwa, ni kile midea kinachoripoti lakini yeye kama yeye hajasema kitu kama hicho,na hizo story ni personal na time hii sio time ya kuwa na beef na mtu

0 comments:

Post a Comment