mtoto
zawadi Godfrey Mwingune mwenye siku 19 kama anavyoonekana akiwa na
macho matatu na uvimbe mkubwa katika paji lake la uso huku kichwani
kukiwa na nundu mfano wa uyoga ambayo inatoa usaa mwingi
Hivi
ndivyo mtato zawadi anavyoonekana kichwa chake uzito wake ni kg 4
na nusu alizaliwa hospitali ya kibena Njombe ni mwenyeji wa Ikengeza
Isimani mkoa wa Iringa
Hapa mtoto zawadi akiwa amejipumzisha katika kitanda
Wazazi
wa mtoto Zawadi Gofrey Mwingune Bw Godfrey Mwingune (30) na mama wa
mtoto huyo Mathar Kitago (28) wakimtazama mtoto wao kwa huzuni mwingi
kutokana na kukosa fedha za matibabu kwa ajili ya kumsafirisha mtoto
huyo kwenda kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa
HUJAFA
hujaumbika ,Mungu ana makusudi yake ni yeye ni muweza wa yote kwani
ndie aliyeumba mbingu na nchi pamoja na viumbe wote wasioonekana na
wanaoonekana hivyo mwacheni Mungu aitwe Mungu,ni kauli ya wazazi wa
mtoto Zawadi Godfrey Mwingune aliyezaliwa akiwa na macho matatu na
kichwa mfano wa uyoga.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mama mzazi wa
mtoto Zawadi Bi .Mathar Kitago (28) mzaliwa wa kijiji cha Kidegembye
Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe alisema kuwa hadi sasa
anamwachia Mungu ambae ndie amempa zawadi ya mtoto huyo.
Kwani
amesema kuwa ilikuwa ni siku ya jumapili January 13 mwaka huu
aliposhikwa na uchungu na kukimbizwa katika kituo cha afya cha
Kidegembye ambako alichukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya wilaya ya
Njombe Kibena kwa matibabu zaidi.
Hata
hivyo alisema baada ya kufika katika Hospitali hiyo aliingizwa
katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa upasuaji na kubahatika kupata
mtoto huyo japo kwa upande wake aliogopa sana baada ya kuonyeshwa
mtoto huyo ila alipiga moyo konde kwa kuwa ni damu yake .
Bi
Mathar mwenye idadi ya watoto watatu sasa akiwemo Zawadi anasema
kuwa mtoto wa kwanza wa kiume ana miaka 9 na mtoto wa pili ni wa
kike ana miaka 4 na wote alijifungua vizuri bila kufanyiwa upasuaji
kama ilivyotokea kwa mtoto Zawadi.
Baba
wa mtoto huyo Bw Godfrey Mwingune ambae anategemea kuendesha maisha
yake kwa kilimo anasema kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Ikengeza
Isimani na kuwa baada ya kupata mtoto huyo wa ajabu aliamua kurejea
nyumbani kwa wazazi wake Igengeza Ismani ili kuwaonyesha mtoto
huyo japo anatambua kuwa mtoto huyo ni zawadi kutoka kwa Mungu na
ndio sababu ya kumpata jina la Zawadi pia.
"
Kweli nilipomleta kwa wazazi kijijini nao wamebaki wakishangaa
kuona mtoto wa ajabu hivyo ila sasa tunafanyaje yote ni mipango ya
Mungu "
Mwingune
alisema kuwa hali ya afya ya mtoto huyo si nzuri kwani mbali ya
kuzawali wa kilo 4 na nusu ila bado anatatizo la uvimbe katika paji lake
la uso pia kichwani kuna kovu kubwa ambalo ni kama ncha mbili hivi
ambalo linatoa usaa mwingi na kuwa jeraha hilo alizaliwa nalo mbali na
vituko hivyo pia alisema katika jicho lake la kushoto kwa juu
kuna jicho la pili na kufanya mtoto huyo kuwa na macho matatu .
Alisema
kuwa tayari mtoto huyo amepata kutibiwa Hospitali ya Kibena
Njombe na Hospitali ya Rufaa Mbeya ila imeshindikana na madaktari
wamemtaka amkimbize katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu
zaidi ama nje ya Tanzania .
Hata
hivyo mzazi huyo anasema kuwa kwa sasa pesa ya haraka inayohitajika
ni kiasi cha Tsh. milioni 1.5 ili kumwezesha kwenda kuanza matibabu
Muhimbili japo gharama za matibabu zinaweza kuongezeka zaidi wakati
kwa upande wake hana uwezo wa kupata hata shilingi 100,000 na
kuwapongeza wakazi wa Isimani ambao wamemchangia kiasi cha shilingi
300,000.
0 comments:
Post a Comment