Kijana ambae amekuwa akiwaliza
watumishi mbali mbali wa umma na watu
binafsi kwa kutumia jina la
waziri wa nchi
ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu
wa bunge kijana
Jonathan
Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)
amekamatwa katika hafla ya
kanisa la
Overcomers FM akitaka kumtapeli waziri mkuu wa zamani
Edward Lowassa kupitia harambee hiyo.
Kijana huyo aliingia katika ukumbi
wa St.DOminic leo katika harambee ambayo mgeni rasmi alikuwa ni
Lowassa na kupita mbele
na kutumia kipaza sauti kuzungumza
kuwa
anaitwa JOnathan Wiliam Lukuvi
na ni mtoto wa waziri wa nchi ofisi
ya waziri mkuu sera na uratibu wa
bunge na kuwa amekuwa akimpigia
simu mara kwa mara Lowassa na hata
katika mkutano wake
wa Jangwani
jijini Dar es Salaam
alipata kuzungumza na Lowassa na hivyo kuomba
kutekelezewa ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na utambulisho huo
baadhi
ya watu waliopata kutapeliwa
na kijana huyo akiwemo mkurugenzi
wa
Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa waliweza kuguna hali iliyopelekea
askari polisi kufunguka na kumtia mbaroni
kijana huyo ambae alikuwa
akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na viongozi
wengine katika
hafla hiyo .
Hata hivyo baada ya polisi kumtia
nguvuni kijana huyo baadhi ya watu
waliotapeliwa waliweza
kumtambua
huku familia ya Lukuvi iliyokuwemo
katika ukumbi huo
ikimkana katu katu
kuwa hana hata chembe ya familia na
watu
hawamtambui .
Kada wa CCM maarufu mkoani Iringa
Godfrey Malenga Lukuvi alisema
kuwa kijana huyo amekuwa
akitumia
jina la waziri Lukuvi kuliza watu na
kuwa wengi wamekuwa
wakilalamika
kuhusu utapeli unaofanywa na kijan
a huyo na kuwa tayari
alipata
kukamatwa na polisi ila alitolewa .
Kwa upande wake katibu
wa mbunge
jimbo la Isimani ambae
pia ni familia ya Lukuvi Bw Thom
Malenga
Lukuvi alisema kuwa amekuwa
akipokea malalamiko mbali mbali kutoka
kwa
watu mbali mbali ambao
wamelizwa na kijana huyo na kuwa
siku zote
alikuwa akiweka mtego
ili kumnasa kijana huyo
tapeli japo
hakufanikiwa kumpata.
Thom ambae yupo nje ya mkoa
wa
Iringa kwa shughuli za kifamilia
alisema kuwa alitamani sana kama
angebahatika kumshuhudia kwa
macho kijana huyo tapeli
ila kwa kuwa
yupo nje ya mkoa
atajitahidi kurudi mapema mjini
Iringa ili kumwona
tapeli huyo.
Kwa upande wake mkurugenzi
wa
Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa Teresia Mahongo
alimweleza mwandishi
wa mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa pia
kijana huyo alipata
kufika ofisini
kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya
kumshtukia
alimtafuta waziri
Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa kijana huyo ni
tapeli mkubwa .
Hata hivyo mwanahabari
Gerald
Malekela wa radio
Nuru Fm alisema kuwa kijana
huyo alipata kufika
studio za
radio hiyo kwa ajili ya kutapeli
uongozi kwa kutumia
jina hilo
na kufika studi za radio hiyo
huku akiwa na barua
inayosifia
watangazaji na kuomba kusaidiwa
zaidi kama mmoja kati ya
wasikilizaji .
Mtandao huu ulipata nafasi ya
kumtafuta kwa njia ya simu
waziri Lukuvi ambae mbali ya
kumkana
kuwa hamtambui
bado alisema kuwa amepata
kuwaliza watu mbali mbali
kwa kutumia jina lake.
Lukuvi alisema kuwa tayari
amepata
kupokea malalamiko
kutoka kwa mkurugenzi wa
Manispaa ya Iringa na
kumwagiza
kumtakata na kutaka sheria ichukue mkondo wake.
"Mimi huyu kijana simtambui na
wala si ndugu yangu ila amekuwa
akitumia jina langu kutapeli watu
na
tayari alikamatwa na polisi kwa utapeli huo"
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt
Christina Ishengoma aliwaonya
watu wanaoendelea kutapeli
wengine
kwa kutumia majina
ya viongozi ama namna nyingine
yeyote kuacha mara
moja na kuwa
akiwa kama mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama
ya
mkoa hatakubali kuona
matapeli hao wakiendelea
kulizwa watu kwa njia
ya udanganyifu .
Hata hivyo aliwataka
wananchi
kujiepusha na wimbo
hilo la utapeli kwa kuwaripoti
polisi watu
wanaowashukia kuwa ni matapeli .
Chanzo: Matukiodaima
|
0 comments:
Post a Comment